Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi amvunja bodi ya wakurugenzi wa shirika la meli na uwakala.


Taarifa iliyotolewa leo Jumanne Novemba 15, 2020 na katibu kiongozi, Dk Abdulhamid Mzee inaeleza kuwa kuvunjwa kwa bodi hiyo kunatokana na Serikali kutoridhishwa na uendeshaji na utendaji wa shirika hilo.


Jana kiongozi huyo alitengua uteuzi wa  katibu wa rais, Suleiman Ahmed Saleh ikiwa umepita mwezi mmoja tangu alipomteua ikielezwa kuwa sasa atapangiwa kazi nyingine.