Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo leo Disemba 20, 2020, ametoa ujumbe kufuatia kifo cha baba yake mzazi mzee Urban Costantine Ndunguru ambaye amefariki dunia Disemba 19, 2020.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Jokate ameandika, ''Kama Baba au Mama yako yu Hai au mtu yoyote wa karibu na thamani kwako, usiache kumwambia UNAMPENDA leo. Huenda ikawa nafasi pekee na ya mwisho kutamka hivyo kwao wakiwa hai. Mungu ni mwema kila wakati. It is well. Upumzike kwa Amani Baba Yetu Mpendwa Mzee Urban Costantine Ndunguru''.


Aidha mwili wa mzee Urban Costantine Ndunguru, unatarajiwa kuagwa Jumatatu Disemba 21, 2020 katika Kanisa la St Peters Dar es salaam, kisha kusafirishwa siku hiyo hiyo kwenda Mbinga Mkoani Ruvuma na mazishi kufanyika Jumanne katika kijiji cha Tanga, Mbinga.