Wasanii wawili wakubwa wa Nigeria Davido na Burna Boy wamedaiwa kupigana katika klabu moja ya burudani nchini Ghana.

Kulingana na BBCPidgin, zogo lilizuka baada ya Burna Boy kuingia katika klabu ambayo Davido alikuwa anawatumbuiza mashabiki wake.

Video iliyovuma mitandaoni inamuonesha Davido aliyekuwa na hasira akizuiliwa na walinzi asipigane.

Hijabainika ni nini hasa kilichosababisha vurugu hizo lakini walioshuhudia wanasema Davido tayari alikuwa katika klabu ya burudan akiendelea na onesho lake.

Lakini baada ya Burna Boy kufika hapo, hali ya taharuki ikatanda. Inadaiwa wasani hao hawapatani.

Licha ya Davido na Burna Boy kulumbana, kuna video nyingine iliyosambazwa mitandaoni inayomuonesha msanii Wizkid akiwa katika eneo la tukio.

Lakini Wizkid hakujihusisha na ugomvi huo badala yake aliendelea na shughuli zake.