Msanii wa muziki Christian Bella amefunguka kwa kuzungumzia tofauti ya ki-brand kati ya wasanii wa Tanzania na wamataifa mengine huku akidai kwamba Fally Ipupa ni mmoja kati ya wasanii wenye mafanikio zaidi Afrika.


Bella amedai Diamond Platnumz ana nyota kali ndio maana muziki wake ni rahisi kupenda kila kona kutokana na juhudi zake za kazi.


Mkali huyo wa masauti ambaye ameachia nyimbo mbili kwa mpigo Tingisha Mguu na Alenda amewataka mashabiki wake kuendelea kufurahia muziki mzuri.

VIDEO: