Mkuu wa benchi la Ufundi kwenye kikosi cha Yanga Cedric Kaze ametoa sababu kujibia ni kwanini mlinda mlango Mkenya Farouk Shikhalo amekuwa akisugua benchi na kuwa chagua la kwanza mbele ya Metacha Mnata.Shikalo ambaye alikuwa kipa bora kwenye ligi kuu nchini Kenya misimu miwili iliyopita na kuwemo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya kilichoshiriki AFCON nchini Misri amekosa nafasi kikosi cha kwanza na kushuhudia Metacha akidaka michezo 15 na yeye akiambulia miwili tu


Hali ya Farouk kusugua benchini imeibua mjadala na wapenzi wengi wa soka wakihoji ni kwanini hasa mlinda mlango huyo aliyekuwa bora awe benchini. Kocha wa Yanga Cedric Kaze amejibia kwa kusema, 


"Shikalo bado ataendelea kuwepo kwenye timu yetu ya Yanga, kwani bado msaada wake unahitajika katika kikosi changu kilichopanga kuchukua ubingwa msimu huu, hiyo ni kutokana na kiwango chake kikubwa alichonacho.


"Shikalo ni kipa mwenye uzoefu mkubwa na pia ni kipa anayeweza kuwachezesha wachezaji wenzake katika mechi, hivyo ni ngumu kumuacha kipa wa aina hii katika timu yangu yenye malengo.


"Kikubwa majeraha ndiyo yaliyomsababishia akapoteza nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, mwanzoni mwa msimu Shikhalo alipata majeraha hivyo akasababisha kupoteza namba katika timu, kwani baada ya kuumia kwake Metacha akaitumia nafasi hiyo kuonyesha kiwango kikubwa na kupata nafasi ya kudumu”.


Ikumbukwe kuwa, Metacha Mnata amecheza michezo 15 ya ligi kuu Bara na kutruhusu bao kwenye michezo 10 na kuwa mlinda mlango pekee kwenye ligi kuu ya TZ Bara kucheza michezo mingi bila wavu wake kuguswa.