Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemteua Maalim Seif Shariff Hamad, kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

Awali chama hicho kikuu cha upinzani kilikataa kuyatambua matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kwa kusema kwamba yalikua batili, hata hivyo chama hicho kimeongeza kwamba baada ya majadiliano ya muda mrefu pamoja na kupokea maoni ya wanachama wake, kimeamua kuungana na serikali ya chama tawala kwa ajili ya kuendesha nchi.