Radi yaua watoto wawili wakike wa familia moja na kuwajeruhi baba na mama wakazi wa kijiji cha Shasya Kata ya halungu kilichopo wilayani mbozi mkoani Songwe katika nyumba tatu tofauti.



Pichani: mfano wa radi

Tukio hilo limetokea majira ya saa saba mchana na kusababisha vifo vya watoto hao waliofahamika kwa majina ya  Edina Mgale, mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Igamba na Miznala Mgale mwenye umri wa miaka minne.

Akielezea tukio hilo baba Mzazi wa Marehemu, Mawazo Mgale amesema walisikia mlio wa radi na baada ya hapo ndipo alipoanza kuita na baadaye kukuta mke wake akiwa amezirai.

”Mimi na mtoto mmoja tulikuwa kwenye nyumba kubwa na marehemu alikuwa kwenye nyumba nyingine mama na watoto wengine walikuwa jikoni na baada ya kusikia mlio wa radi ndipo nilianza kuita na kukuta mama amezirai” amesema Mawazo Mgale

Nae diwani wa kata ya Halungu Maalifa Mwashitete,amewatoa hofu wananchi kuacha kuhusisha tukio hilo na imani za kishirikina.