Mzee Mohammed Fungafunga maarufu katika tasnia ya filamu kama "Jengua" amefariki dunia leo Desemba 15, Mkuranga mkoani Pwani baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa taarifa, Marehemu Jengua alikua akisumbuliwa na Maradhi ya Kupararaizi.

udaku tunatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki pamoja na wanatasnia wote kwa ujumla kwa kuondokewa na mkongwe huyo wa filamu nchini.

#Tanzia