Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi, amemuapisha, Maalim Seif Sharif Hamad kuwa Makamu wa Kwanza wa rais kutoka Chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo.

Hafla ya uapishwaji imefanyika leo Desemba 8, Ikulu Zanzibar.

Hii inakuwa ni mara ya pili kwa kiongozi huyo mkongwe kushika wadhfa huo kwani mwaka 2010 hadi 2015. Wakati wa uongozi wa Dk. Ali Mohammed Shein, alihudumu kwenye nafasi hiyo na sasa anahudumu kwenye serikali ya Nane chini ya Dk. Mwinyi.