Huruma Mjumbe (54) Mkazi wa Mbagala Mwanatoli, amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kumlawiti binti yake mwenye miaka 11


Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Kasimu Mushi amesema, Huruma alikabiliwa na kosa la kubaka na kumuingilia kinyume na Maumbile mtoto huyo kati ya Januari 2017 na Februari 19, 2019 huko Mbagala Mwanamtoli

Ushahidi wa daktari umeithibitishia Mahakama pasi na shaka kwa ukatili huo ulifanyika na adhabu hiyo imetolewa ili liwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo