Mkazi wa Mbagala, Faraji Omary amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akikabiliwa na makosa manne likiwemo la kuchapisha picha chafu za ngono.

Omary(26), amefikishwa mahakamani hapo leo Desemba 29, na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu.

Awali, Wakili wa Serikali, Adolf Ulaya akisoma hati ya mashtaka amedai kuwa, mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka manne ambayo ni kuchapisha ponografia, kusambaza maudhui machafu, kusambaza picha chafu na kukutwa na machapisho yenye maneno machafu.

Wakili Ulaya aliendelea kudai, shtaka la kwaza ni kuwa kati ya Desemba 4 na 14, mwaka huu jijini Dar es Salaam mshtakiwa alituma video na picha za ponografia kupitia WhatsApp.

Katika shtaka la pili, Wakili amedai kati Desemba 10, mwaka huu na Desemba 12, mwaka huu eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam mshtakiwa alitengeneza tiketi zenye maneno machafu yanayoharibu maadili ya umma.

Shtaka la tatu Wakili Ulaya ameendelea kudai Desemba 12, mwaka huu eneo la kariakoo jijini Dar-es-Salaam mshtakiwa alitengeneza tiketi zenye maneno machafu kwa ajili ya kufanya biashara na mtu aliyejulikana kwa jina la, Aisha Feruz.

Mshtakiwa amekana kutenda makosa hayo nakurudishwa rumande hadi Januari 11, 2021 baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili wenye kusaini hati ya Sh 5,000,000 kila mmoja sambamba na barua za utambulisho