EMMANUEL Okwi mshambuliaji wa kikosi cha Al-Ittihad ya Misri amekutwa na Virusi vya Corona hivyo atakosa mechi kadhaa ndani ya Ligi Kuu ya Misri.


Raia huyo wa Uganda ambaye amecheza pia Ligi Kuu Bara ambapo alicheza ndani ya Simba kwa wakati tofauti pia alicheza kikosi cha Yanga atakosa mchezo pia dhidi ya Pyramids FC baada ya kukutwa na Corona.

Mabosi wa Al-Ittihad wamethibitisha kwamba Okwi ana Corona na hayupo nchini Misri kwa sasa bado yupo Uganda.

"Safari ya kurejea kwa mshambuliaji wetu ambaye anacheza timu ya taifa ya Uganda imesimamishwa baadaye kukutwa na Corona.

"Matokeo hayo ameyapata akiwa nchini Uganda kwani bado hajarejea nchini Msiri nasi tunamuombea apone haraka," ilieleza taarifa ya klabu. 

Okwi alikuwa na kikosi cha timu ya taifa ya Uganda kilichokuwa zikisaka tiketi ya kufuzu Afcon ambapo timu yao ipo kundi B.