MENEJA wa mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz, Hamisi Taletale ‘Babu Tale’ amejitokeza na kulisafisha jina lake baada ya kupakwa tope na baadhi ya mahasidi wake.

Tale ambaye ni mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, alikashifiwa na baadhi ya mashabiki  katika mitandaoni ya kijamii wakidai kuwa amemtoa mkewe kafara ili aweze kushinda wadhifa huo.

Akizungumza na Kituo cha radio cha Cloud FM, Babu Tale amesema alikuwa anampenda sana mkewe na kamwe hakuwahi hata siku moja kuwazia kufanya jambo la hovyo kama hilo.

“Watu wanasema kwamba nilimuua mke wangu kwa kumtoa kafara, hii yote ni propaganda tu. Mimi nilimpenda sana mke wangu na nisingefanya jambo lolote la kuvunja ndoa yangu, tulipendana sana,” amesema Tale.

Pia amedai kwamba hadi wa leo, kitendo cha kumkoa mkewe, kinampa mawazo na wakati mwingine hujikuta akilia na kumwaga machozi akimuuliza Mungu kwa nini alichukua ubavu wake.

Kulingana na Tale, anaheshimu sana ndoa na hakuna lolote lingemfanya amtoe mkewe kafara. Mkewe Tale Shamsa alifariki ghafla dunia mwezi Juni mwaka huu baada ya kuugua kwa muda mfupi.