Kikosi cha Arsenal kimeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Chelsea.
Mchezo wa leo wa Ligi Kuu England Uwanja wa Emirates imewafanya mashabiki wa timu hiyo kuwa na furaha kwa kuwa walikosa ushindi kwa muda mrefu baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Manchester United.
Mabao ya Arsenal inayonolewa na Mikel Arteta yalifungwa na Alexandre Lacazette dk 34 kwa mkwaju wa penalti, Granit Xhaka dk 44 na Bukayo Saka dk 56
Kwa Chelsea inayonolewa na Kocha Mkuu, Frank Lampard bao lilifungwa na Tammy Abraham dakika ya 85.