DAWA ya moto ni moto! Baada ya staa wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ kumletea ‘mapichapicha’ aliyekuwa mkewe, Sarah Michelotti, upepo umegeuka na bibie unaambia anakamilisha mchakato wa kumfi lisi mumewe huyo wa zamani, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA limedokezwa.

 

HARMO ALIANZA…

Wikiendi iliyopita, Harmonize au Harmo ndiye aliyeanza kuchafua hali ya hewa baada ya kuandika waraka kwenye ukurasa wake wa Instagram kumuomba radhi mwanaye mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi saba kwa kutomtunza kwa kuhofi a kutibua ndoa yake na Sarah.

 

UJUMBE WENYEWE…

“Ukweli humuweka yeyote huru, haijalishi ni kiasi gani au muda gani, ila ninaamini kusema hili litafanya moyo wangu uwe huru na kujiona muungwana, mbele ya Mungu na kwa mtoto wangu kipenzi, my fi rst love Zuu. “I’m so sorry my Princess for not ever been proud of you for one year and seven months.

 

“Nisamehe pia kwa kutokuwa na muda na wewe hata kukuangalia pale ulipokuwa unaumwa, kwa kuhofi a mahusiano ambayo nayaheshimu sana…” Alisindikiza ujumbe huo chini ya picha inayomuonesha yeye akiwa na binti yake huyo katika pozi tofauti. BIBIE AKINUKISHA Baada ya Harmo kushusha waraka huo ndipo Sarah naye alipojivisha mabomu kama yote na kuanza kulipuka kama hana akili nzuri.

 

ADAI KUMWEZESHA

Kwenye maelezo yake, Sarah alimwaga mboga kwa kusema yeye ndiye aliyekuwa akimwezesha Harmo kwa kila kitu. AZUNGUMZIA MTOTO Kama hiyo haitoshi, bibie alisema hata suala la huyo mtoto si la kweli kwani kiuhalisia wakiwa kwenye ndoa walishapima kipimo cha vinasaba (DNA) na majibu yalionesha wazi kuwa si mwanaye hivyo anamshangaa kujinasibu sasa kuwa ni mwanaye.

 

FULU MAPICHAPICHA

Katika kuonesha kwamba anachozungumza anamaanisha, Sarah alitupia vipimo ambavyo vinaonesha kuwa ni vya DNA vikionesha kuwa mtoto si wa Harmo (negative). Vipimo hivyo viliitaja moja ya hospitali kubwa jijini Dar kwamba ndiyo iliyompima na kutoa majibu hayo.

 

SIRI YAVUJA…

Kufuatia waraka mbalimbali zilizoporomoshwa na Sarah, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA lilitonywa na mtu wa karibu na mke huyo wa zamani wa Harmo kuwa tayari ameshaweka mambo sawa ili kumburuza jamaa huyo mahakamani.

 

“Harmo ameshafi lisika mpaka dakika hii maana si unajua pesa zote bibie ndiye aliyekuwa mwezeshaji na ukizingatia zote zilikuwa kwenye maandishi ikiwemo zile shilingi milioni 500 alizomlipia wakati anajitoa Lebo ya Wasafi Classic Baby,” kilidai chanzo hicho na kuongeza;

“Sasa kama hizo atatakiwa kuzirejesha, bado kuna Konde Gang (ofi si zilizopo Mbezi-Beach, Dar) na magari unadhani Harmo atabaki na nini kama siyo kumuua mtoto wa watu na presha ya kufi lika?”

 

HARMO ALIKIRI…

Kabla mambo hayajakorogeka, Harmo mwenyewe amekuwa akikiri mara kadhaa kupata sapoti kubwa kutoka kwa Sarah na hata kwenye wimbo wake wa Never Give Up amemshukuru mwanadada huyo ambaye ni raia wa nchini Italia.

 

MENEJA AFUNGUKIA KUFILISIKA

Gazeti la IJUMAA WIKIENDA lilifanya mazungumzo na meneja wa msanii huyo, Beauty Mmari ‘Mjerumani’ ambapo alipoulizwa kuhusu ishu ya msanii wake huyo kufi lisika, alisema siyo rahisi kwa sababu anapambana kila kukicha.

 

“Harmo ni msanii ambaye anapambana sana ili kuhakikisha anafanya kazi nzuri sasa sidhani kama anaweza kushuka kwa sababu ya mwanamke,” alisema Mjerumani kisha kukata simu.

 

TUMEFIKAJE HAPA?

Harmo na Sarah waliishi kwenye uchumba kwa muda mrefu kabla ya kufunga ndoa ya kimila nyumbani kwa wazazi wa mrembo huyo nchini Italia.

 

Kama hiyo haitoshi, wawili hao waliporejea jijini Dar walifanya bonge la sherehe kisha kuanza kuishi kama mke na mume hadi pale walipopishana na kumwagana.

 

Hivi karibuni, Harmo alidaiwa kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji wa Bongo Movies, Kajala Masanja ambaye inaelezwa ndipo anapopoozea machungu mpaka sasa.