SEXLADY kunako gemu ya fasheni Bongo, Hamisa Mobeto kwa mara nyingine ameingia kwenye vichwa vya habari baada ya mpenzi wake wa zamani aliyefahami kwa jina moja la Alex kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake Tahiya John.

 

Ishu hiyo ilianza kusambaa kama moto wa kifuu wiki iliyopita baada ya mwanadada huyo kuposti picha akiwa na mchumba wake huyo, huku akiwa na pete kidoleni.

 

Pia katika akaunti ya Instagram ya mrembo huyo amebadilisha ‘profile’ yake na kuandika ‘taken’ akiwa na maana ya kwamba tayari ni mchumba wa mtu, huku Alex naye akiwa amefanya vivyo hivyo.

 

“Ama kweli subira yavuta kheri, huyu si ndo yule alikusaliti na Mobeto? Mmmmh! Haya bwana hongera kwa kuvumilia Mungu alikuandikia wewe na sio huyo (tusi),” alikomenti shabiki mmoja kwenye posti ya mrembo huyo.

 

TUJIKUMBUSHE

Zaidi ya miaka minne mwanamama Hamisa aliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mfanyabiashara maarufu Bongo, Francis Ciza ‘Majizzo’ na kufanikiwa kuzaa naye mtoto mmoja wa kike ajulikanaye kwa jina la Fantancy.

 

Hata hivyo, penzi lao halikuchukua muda mrefu wakabwagana na mwanaume huyo akamvalisha pete ya uchumba msanii wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.

 

Baada ya kumwagana na Majizzo, Mobeto akaingia kwenye penzi jipya na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na kufanikiwa kupata naye mtoto mmoja wa kiume anayefahamika kwa jina la Dylan.

 

Wawili hawa walifanya mapenzi yao kuwa ya siri kubwa na baadae wakabwagana na sasa kila mmoja ana maisha yake.

 

Mobeto akaona kukaa singo hawezi ghafla tukasikia ameingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mfanyabishara anayedaiwa kuwa na mkwanja wake mjini Alex huku madai ya chinichini yakidai kuwa mwanaume huyo alimuiba kwa mrembo Tahiya na vita yake ikawa si ya kitoto.

 

Wakati mambo yote hayo yakiendelea Mobeto, aliziba masikio na kuendelea kubanjuka kiaina na bwana wa mwenzake, lakini ndio hivyo penzi lao halikudumu baada ya miezi kadhaa wakabwagana na sasa mwanaume huyo amemrudia mpenzi wake na kumchumbia mazima.

STORI | MEMORISE RICHARD, RISASI