Kumekuwa na sintofahamu kubwa kuhusu uwepo wa ujauzito kwa msanii wa BongoFleva Amber Lulu, na stori za mitandaoni zilidai alikuwa na mahusiano na Uchebe na P Funk Majani kwa hiyo mmoja wapo huenda akawa muhusika wa ujauzito huo.

 

Sasa msanii wa zamani wa kundi la BOB Micharazo ambaye ndiyo anayedaiwa kumpa ujauzito msanii huyo amefunguka kusema bado haijawa rasmi kuzungumzia suala hilo ila yote ni mipango na baraka za Mungu.


Akifunguka zaidi kuhusiana na hilo Emba Bosion amesema kuwa "Nisingependa niongelee rasmi hilo suala Amber Lulu mwenyewe ndiyo atanyoosha, hizo zote ni baraka za Mwenyezi Mungu Inshaalah na Mungu mkubwa" 


Emba Bosion ambaye ametoka nyuma ya nondo kwa sasa ni msanii anayepata usaidizi wa kimuziki chini ya Q Chief na tayari ameachia kazi mpya inayoitwa nyota akimshirikisha Billnass na Q Chief.