Ni Headlines za mwigizaji Wema Sepetu ambae hivi karibuni aliwahi kufanyiwa mahojiano kwenye na akazungumzia kuhusu video iliyowahi kuvuja ikimuonesha akiwa na mwanamke, sasa Ayo TV & millardayo.com imefanikiwa kumpata PCK ambae anahusishwa katika sakata hilo.


PCK Aliweza kufunguka na kueleza mwanzo mwisho wa uhusiano wake na mwigizaji Wema Sepetu ‘Hata tukitazama ile video ilirekodiwa na Wema mwenyewe na mimi sikujua kama yatakuja kutokea yale yaliyotokea , na nilikuwa tayari  nilikuwa nimesha kwa wazazi wangu’– PCK


‘Sijawahi kumkosea Wema hata kidogo na kile kinachoendelea  mitandaoni kwamba nilimchukua Pesa na  kama ana ushahidi wowote basi niko tayari kuilipa hiyo Pesa wala sijamtapeli , aache kutumia watu wa mitandaoni kunichafua mimi, kuna vitu vingi watu hawajui mimi na Wema tulikuwa na malengo gani ya maisha’- PCK