Hili game linaweza kusitisha mkataba wako wa kuwa superstar ukianza kutoa ngoma kwa kusua sua mashabiki wanahamia kwengine.

Sijui ni kipi kinaendelea lakini Ali amepoa mno, Yale ya "unikome" ulitushangaza sana ila tukavunga tu maana ni mambo binafsi katika maisha ya binadamu, hatujakaa sawa tunaskia producer mkali mMan Walter anakulalamikia hujamlipa studio na kaapa hataki kufanya kazi na wewe, Kaka nini shida lakini? Utapotea kiutani utani hivi hivi na kutuachia maumivu mashabiki zako.

Kitu kingine nakuchana live japo mimi ni shabiki, ACHA DHARAU NA MARINGO BRO! Ukiachana na matukio kadha wa kadha yanayoashiria tabia hizi, Ile siku uliyokusanya waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa ngoma ya mshumaa nahisi ulikataa mawazo ya wengine, matokeo yake ukalikoroga mwenyewe ukaonekana huwezi kuongea mbele ya watu, hata ngoma ya mshumaa haikupata mwamko.

Bora kuchelewa kubadilika kuliko kukataa kabisa mabadiliko, mashabiki wako tupo bado na tupo tayari kukupa sapoti ya kukufanyavuwe juu zaidi.


By Machozi Ya Simba