Baada ya zaidi ya miaka 50 ya kuhudumu katika ofisi ya umma, na azma ya muda mrefu ya kutaka kuwa rais, Joe Biden hatimaye amepata idhini ya raia wa Marekani kuhudumu katika Ikulu ya White House.

Haikuwa kampeni iliyobashiriwa na mtu yeyote.

Ilifanyika kati kati ya janga la corona na maandamano makubwa ya kupigania haki ya jamii ya Wamarekani weusi.

Alikuwa anamenyana na kiongozi ambaye sio wa kawaida. Mtangulizi ambaye amekataa kukubali kushindwa.

Lakini katika jaribio lake la tatu kugombea urais wa Marekani, Biden na timu yake wamepata njia ya kukwepa vihunzi vya kisiasa na kupata ushindi, licha ya kinyang’anyiro kikali cha kupata kura ya wajumbe , bwana Biden alimshinda Trump kwa mamilioni ya kuraza kitaifa.

Hizi hapa sababu tano kwa nini mwana huyu wa muuzaji magari kutoka Delaware hatimaye alishinda uchaguzi wa urais.

1. Covid, Covid, Covid

Huenda hii ndio iliyokuwa sababu kubwa iliyomfanya Biden kushinda uchaguzi japo hakuwa na uwezo wa kudhibiti hali ilivyokuwa.

Janga la corona ambalo limesbabisha vifo vya watu 230,000, pia limebadilisha maisha ya Wamarekani na siasa za mwaka 2020 siku za mwisho za kampeni ya uchaguzi mkuu.

Donald Trump mwenyewe alionekana kukubaliana na hilo.

“Kutokana na taarifa gushi kila kitu ni Covid, Covid, Covid, Covid,” rais alisema katika mkutano wa kampeni wiki iliyopita mjini Wisconsin, ambako visa vya maambukizo ya virusi vya corona vimeongezeka katika siku za hivi karibuni.

Biden na Trump

Hatua ya vyombo vya hapari kuangazia zaidi ugonjwa wa Covid, hata hivyo ilikuwa mtazamo ambao hushawishi mafikira ya watu kuhusu janga la corona- hali ambayo ilikuwa na matokeo ambayo hayakuegemea upande wowote katika kura ya maoni kuhusu jinsi rais alivyoshughulikia janga la corona.

Utafiti uliyofanywa mwezi uliopita na kituo cha utafiti cha Pew, uliashiria kuwa Biden alikuwa mbele ya Trump kwa asilimia 17 linapokuja suala la kujiamini katika uwezo wao wa kukabiliana na mlipuko wa virusi vya corona.

Janga hilo na baadaye kushuka kwa viwango vya uchumi ilimlazimu Trump kuacha kutumia kauli mbiu yake ya ukuaji na ustawi katika kampeini.

Pia iliangazia jinsi baadhi ya Wamarekani walivyosikia kuhusu uongozi wake kupitia ukosefu wa mwelekeo wa utawala wake kukinzana na masuala ya kisayansi jinsi ya kushughulikia masuala ya sera yawe madogo au makubwa na ni yapi yapewe umuhimu bila upendeleo.

Janga la corona liliongoza katika kuamua uwezo wa Trump, kwa mujibu wa Gallup, ulishuka kwa asilimia 38 wakati mmoja msimu wa joto – suala ambalo Biden alitumia kuimarisha Kampeni yake.

2. Kampeni ambayo haikugharimu hela nyingi

Katika kipindi cha uongozi wake wa kisiasa Biden, alijijengea sifa ya kujiingiza kwenye matatizo kutokana na matamshi yake ya kiholela.

Hali hiyo ilirudisha nyuma kampeni yake ya urais mwaka 1987, ilimsaidia kujitathmini tena makosa hayo alipogombea tena urais mwaka 2007.

Katika jaribio lake la tatu kuingia Ikulu ya White House, Biden bado alikabiliwa na mitego ya matamshi lakini ilikuwa sahali illkilinganishwa na hali ilivyokuwa miaka iliyopita.

Sehemu iliyosaidia kukabiliana na changamoto hiyo ni kwamba rais mwenyewe alikuwa chanzo cha habari katika mzunguko wa matukio yaliyogonga vichwa vya habari.

Biden na Trump

Sababu nyingine ni kuangaziwa kwa taarifa zingine kuu kama vile – janga la corona, maandamano yalifuatia kifo cha George Floyd na kukatizwa kwa shughuli za kiuchumi – ambazo zilivutia umuhimu wa kitaifa.

Lakini kampeni ya Biden ilijipatia umaarufu wa kuhakikisha mgombea wao hajihusishi na mkusanyiko wa watu, kudhibiti kampeni kwa kasi inayostahili na kupunguza uwezekano wa uchovu au kufanya mambo bila mpangilio ambao huenda ukaleta shida.

Pengine katika uchaguzi wa kawaida, ambapo Wamarekani hawakuwa na hofu kuhusu maambukizi ya virusi vya corona , huenda mpango huo ungeligonga mwamba.

Kampeni hiyo ilihakikisha inatoa nafasi kwa Trump kuendelea kutumia mdomo wake kujihujumu – na bila shaka ilizaa matunda.

3. Mtu mwingine yeyote na sio Trump

Wiki moja kabla ya siku ya uchaguzi, kampeni ya Biden ilizindua matangazo ya biashara ya televisheni iliyokuwa na ujumbe ambao ulikuwa sawa na ule ulitolewa mwanzo wa kampeni mwaka jana, na hotuba yake ya kukubali uteuzi mwezi Agosti.

Uchaguzi huo ulikuwa “mashindano ya kuokoa Marekani” , na nafasi ya kitaifa ya kukomesha kile alichotaja kuwa mgawanyiko na vurugu zilizoshuhudiwa miaka minne iliyopita nyuma, alisema.

Uchaguzi ulibadilika na kuwa kura ya maoni dhidi ya Trump

Chini ya kauli mbiu hiyo kulikuwa na ujumbe wenye maana fiche.

Biden alitumia tajiriba yake ya kisiasa kuwasilisha ujumbe kwamba Trump alikuwa anatumia kauli za chuki zinazogawanya watu, na kwamba raia wa Marekani wanataka uongozi uliotulia na wenye busara.

“Nimechoshwa na mtazamo wa Trump,” anasema Thierry Adams, mzaliwa wa Ufaransa ambaye amepiga kura kwa mara ya kwanza baada ya kuishi kwa miaka 18 Florida kushiriki katika shughuli ya uchaguzi wa urais mjini Miami wiki iliyopita.

Democrats walifanikiwa kuufanya uchaguzi huu kama kura ya maoni dhidi ya Trump na wala sio uchaguzi kati ya wagombea wawili wakuu.

Ujumbe wa ushindi wa Biden ulikuwa “sio Trump”. Jambo lililotumiwa zaidi na Democrats ni kwamba ushindi wa Biden ulimaanisha Wamarekani watatulia kwa wiki kadhaa bila kufikiria siasa.

Ilitumiwa kama utani lakini kwa kiwango fulani ilikuwa na ukweli.

4. Kusalia na mpango wake

Wakati wa kampeni mgombea wa Democratic, Joe Biden alikabiliwa na ushindani kutoka wapinzani wake Bernie Sanders na Elizabeth Warren ambao waliendesha kampeni iliyofadhiliwa na kupangwa vyema iliyovutia umati wa watu.

Licha ya ushindani kutoka kwa wagombea wa kiliberali Biden alisalia na mpago wake wa zamani, kukataa kuunga mkono bima ya afya kwa wote inayoendeshwa na serikali, elimu ya taasisi ya juu bila malipo au kadi ya utajiri.

Hatua hii ilimwezesha kuwashawishi watu wenye misimamo ya kadri na Warepublican ambao hawajaathiriwa wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu.

Mpango huo ulionekana kupitia uamuzi wa Biden kumteua Kamala Harris kuwa mgombea mwenza wake wakati alikuwa na nafasi ya kumteua mtu ambaye angelipata uungwaji mkono kutoka kwa wapinzani wa ndani ya chama.

Sehemu moja ambayo Biden aliwakaribia Sanders na Warren ilikuwa katika masuala ya mazingira na mabadiliko ya tabia nchi – pengine katika kuwahamasisha wapiga kura vijana umuhimu wa masuala hayo katika ulimwengu wa sasa na ule ujao.

5. Pesa zaidi, matatizo machache

Mapema mwaka huu, kampeni ya Biden iliishiwa na fedha.

Aliingia katika kampeni ya uchaguzi akiwa katika hali ngumu akilinganishwa na Trump, ambaye alikuwa ametumia fedha zote alizojikusanyia katika muhula wake wa kwanza ambazo zilikuwa zinakaribia mabilioni ya dola.

Kuanzia mwezi Aprili, hatahivyo ,kampeni ya Biden ilijiimarisha kupitia michango ya umma na kuwa madhubuti kifedha ikilinganishwa na wapinzani wao.

Mwanzo wa mwezi Oktoba, kampeni ya Biden ilikuwa na pesa taslimu dola milioni 144 kuliko Trump, walizotumia kuzika Warepublican kwenye kaburi la sahau kupitia matangazo ya televisheni katika majimbo yaliyokuwa na ushindani mkali.

Mfuasi wa Biden Texas

Pesa sio kila kitu bila shaka. Miaka minne iliyopita kampeni ya Clinton ilikuwa na pesa kiasi cha haja kuliko kampeni ya Trump.

Lakini mwaka 2020, wakati kampeni zilidhibitiwa na janga la corona – raia walianza kufuatilia taarifa za kampeni kupitia vyombo vya habari majumbani mwao, Biden alitumia fedha alizokuwa nazo kuwafikia wapiga kura kupitia ujumbe wa kuwahamasisha wafuasi wake kujitokeza kumpigia kura kwa wingi hadi siku ya mwisho ya kampeni.

https://www.instagram.com/tv/CHZhv5ehlWU/

https://www.instagram.com/tv/CHZhv5ehlWU/

Credit BBC.

The post Zifahamu Sababu tano kubwa zilizomfana Biden kumshinda Trump Urais (+Video) appeared first on Bongo5.com.