Mzazi  mweza wa Msanii Nasib Abdul  ‘Diamond Platunumz’   ambaye ni raia wa Uganda Zari Hassan maarufu  ‘Zari the Boss Lady’ ametua Bongo na watoto wake Princess Tiffah na Prince Nillan usiku wa jana, akitokea nchini Afrika ya Kusini yalipo makazi yake.

Zari alipokelewa na Diamond ambaye alionekana mwenye furaha baada ya kupita miaka miwili tangu aione familia yake.

Akiongea na wana habari Zari amesema amekuja kwa ajili ya  watoto kumwona baba yao,” walikuwa wanataka kumuona baba yao lakini hasa Diamond ndio alikuwa na hamu zaidi ya kuwaona”.

Alipulizwa kuwa wamerudiana alikataa na kusisitiza kuwa wao ni wazazi wapo kwa ajili ya kuwapa furaha watoto wao na sio vinginevyo.

Diamond na Zari waliingia kwenye mahusiano mwaka 2014 na kudumu kwa  miaka minne hadi 2018 Zari alipotangaza kuwa mahusianoyao yamevunjika akimtaja Diamond kama chanzo kwa kutokuwa mwaminifu akidaiwa kuwa alim ‘cheat’ na wasichana kadhaa akiwemo Hamisa Mobeto.