Watahiniwa 646,148 wanatarajia kuanza Mitihani hiyo leo hadi Novemba 20, 2020. Kati yao 301,831 (46.71%) ni Wavulana huku 344,317 (53.29%) wakiwa Wasichana.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dkt. Charles Msonde amesema idadi hiyo ni ongezeko la 5.7% ikilinganishwa na waliofanya mitihani hiyo mwaka jana.
Aidha, ameeleza kuwa Mitihani ya Darasa la Nne itafanyika Novemba 25 na 26, ambapo idadi ya Wanafunzi waliosajiliwa ni 1,825,679 wakiwemo Wavulana 909,068 na Wasichana 916,611.
The post Zaidi ya watahiniwa laki sita wa kidato cha pili Tanzania nzima, wameanza mitihani appeared first on Bongo5.com.