Mkurugenzi wa Utafiti na Huduma za Uuguzi na Oparesheni wa Hospitali ya Shree Hindu Mandal Kishan Mistry akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na huduma wanazozitoa za upimaji na ushauri bure katika wiki ya Maadhimisho ya Magonjwa Yasiyoyakuambukiza jijini Dar es Salaam.
Mmoja ya mwananchi akipata huduma ya macho katika hospital ya Shree Hindu Mandal katika Maadhimisho ya Wiki ya Magonjwa Yasiyoyakuambukiza.
Mkazi wa Gongolamboto Philmont Matiko akizungumza namna alivyopata huduma katika Hospital ya Shree Hindu Mandal katika Maadhimisho ya Magonjwa Yasiyoyakuambukiza jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wananchi wakipata huduma na ushauri bure katika hospitali ya Shree Hindu Mandal jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

HOSPITALI ya Shree Hindu Mandal imesema katika kuadhimisha Wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoyakumbukiza watatoa huduma za bure za kupima na kutoa ushauri kwa wananchi wataokwenda katika hospitali
hiyo.

Huduma wanazozitoa katika maadhimisho kwa vipimo na ushauri ni  magonjwa ya Kisukari, Kansa, Shinikizo la damu (BP)  na huduma za macho ambapo katika magonjwa hayo yapo mengine ni ushauri  na kubadili mfumo wa kuishi baada ya kuonekana na viashiria vya ugonjwa.

Akizungumza wakati wa  maadhimisho hayo kwa niaba Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Shree Hindu Mandal Mkurugenzi wa Utafiti za Huduma  za Uuguzi na Oparesheni Kishan Mistry amesema katika maadhimisho hayo Manispaa ya Ilala ndio imeipa jukumu hospitali hiyo kutoa huduma za kupima magonjwa mbalimbali kwa siku tatu mfululizo na kuungana na serikali  siku ya Alhamis  hadi Jumamosi kwa kutoa huduma  katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Mistry amesema kuwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam wajitokeze kwa wingi katika hospitali hiyo  kupata vipimo pamoja na ushauri katika magonjwa yasiyoyakuambikiza kwani wakati mwingine mtu anaweza kuhisi mzima kumbe ana tatizo ambalo likiibuka linakuwa ni shida.

Muuguzi wa Mshauri wa Ugonjwa wa Kisukari wa Hospitali ya Shree Hindu Mandal Mary Nghumbu amesema kuwa ugonjwa wa kisukari kina mambo mawili moja ni kurithi na pili mfumo wa maisha unaotokana ulaji uliopitiliza kwa mahitaji ya mwili usiozingatia lishe.

Amesema kuwa katika kuepukana na tishio la ugonjwa wa kisukuri  pamoja na shinikizo la damu njia rahisi ni kufanya mazoezi mara kwa mara kuepukana na vyakula vya mafuta yaliyokupitilizta na kuzingatia ulaji unafuata lishe kwa kuzingatia mpangilio wa chakula.

Mkazi wa Gongolamboto Philimon Matiko amesema utaratibu wa Hospitali hiyo kutoa huduma na vipimo ni suala la kujenga uimara kwa afya za watanzania na kushauri kufika vijijini.