Mtandao wa WhatsApp umebadili baadhi ya mifumo yake, sasa unawawezesha Watumiaji wake kutuma ujumbe ambao unaotoweka baada ya muda fulani kwa lengo la kuwawezesha kuondoa nyayo zao za kidijitali.
Maboresho hayo yameanza kwa waliofanya ‘Update’ zilizokuwepo tangu Alhamisi na watumiaji wataweza kuweka chaguo kwenye ujumbe wowote, kwa mtu mmoja au kundi na ujumbe utajifuta wenyewe baada ya siku 7 tangu kutumwa.
Wahusika wamesema kuwa “Tunaanza na siku saba kwa sababu tunafikiria inatoa wasaa kwa mtumiaji kufikiria kile alichokituma au kiandika kwa mwingine na hata kwa yale mazungumzo ambayo sio ya kudumu kwahiyo ndani ya siku saba hata kama mtu alichelewa kusoma ujumbe au ni msahaulifu kwa siku hizo atakuwa ameisoma meseji au hatasahau hata kama ujumbe ukifutwa”
“Ingawa ni nzuri kubaki na kumbukumbu kutoka kwa marafiki na familia, lakini pia mengi ya yale tunayotuma hayahitaji kuwa ya milele. Lengo letu ni kufanya mazungumzo kwenye WhatsApp wahisi ukaribu iwezekanavyo, hsa kwa wale ambao hawapaswi kukaa karibu milele, sidhani kama mazungumzo yote utapenda yabaki hasa yale ya siri kama mmezungumza na mmemaliza haina haja ya kuendelea kubaki”
https://www.instagram.com/tv/CHPjAjbhGz-/
https://www.instagram.com/tv/CHPjAjbhGz-/
The post WhatsApp: Sasa unaweza kutuma ujumbe na kuweza kuufuta ndani ya siku 7 (+ Video) appeared first on Bongo5.com.