Watoto wawili wa kike wameokolewa kutoka kwenye kifusi cha jengo lililoanguka siku tatu baada ya kutokea tetemeko la ardhi lililosababisha vifo vya watu kadhaa katika pwani ya Uturuki na katika visiwa vya Uigiriki kwenye Bahari ya Aegean.

Hadi kufikia sasa idadi ya watu waliokufa ni 87 baada ya miili zaidi kupatikana katika mji wa Izmir nchini Uturuki.

Shirika la habari la Uturuki, Anadolu limesema saa saba zilizopita mtoto wa kike wa miaka 3 aliokolewa kutoka kwenye kifusi.

Mama yake na dada zake wawili waliokolewa siku mbili zilizopita. Maafisa wameelezea kwamba watu 220 waliojeruhiwa bado wanatibiwa hospitalini, wanne kati yao wakiwa mahututi.

Karibu watu 1,000 walijeruhiwa wengi wao kutoka Uturuki baada ya kutokea tetemeko hilo la ardhi katika pwani ya Uturuki na katika kisiwa cha Ugiriki cha Samos.

The post Wawili waokolewa kwenye kifusi baada ya tetemeko Uturuki appeared first on Bongo5.com.