Samirah Yusuph
Busega. Watu watatu wakazi wa wilaya ya Busega Mkoani Simiyu ambao ni wavuvi katika ziwa victoria wamekufa maji kwa kuzama maji baada ya mtumbwi waliokuwa wanautumia katika shughuri zao kupasauka.

Tukio hilo limetokea jana tarehe 29 mwezi wa 11 katika kata ya Kabita tarafa ya Busega wakati wavuvi hao wakiwa wanaendelea na shughuli zao za uvuvi kama kawaida.

Ambapo kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu Richard Abwao aliwaambia waandishi wa habari kuwa kwa mujibu wa taarifa ya daktari aliyechunguza miili hiyo kifo chao kilitokana na kunywa maji mengi na kukosa hewa na kuonngeza kuwa:

"Waliokufa maji ni Mnaga Manyama miaka 28, Kulwa Juma miaka 15 na Bitulo Manyama wote wakazi wa Kabita wilayani Busega.

Aidha tukio hilo lilitokea baada ya mtumbwi waliokuwa wanatumia kuzama kufuatia mtumbwi huo kupasuka na kuanza kuingiza maji." Alisema Abwao.

Huku akitoa wito kwa wananchi wanaofanya shughuli za uvuvi kufanya ukaguzi na matengenezo hitajika ya vifaa vyao mara kwa mara.

Mwisho.