Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora linawashikilia watoto 11, ambao ni wanafunzi wa shule za msingi kwa tuhuma mbalimbali za uvunjaji, uporaji na unyang’anyi wa kutumia nguvu na silaha katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Tabora mjini na kwamba walivunja nyumba ya Askari mstaafu na kuiba.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, ACP Barnabas Mwakalukwa.

Kauli hiyo imetolewa hii leo Novemba 6, 2020, na Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Barnabas Mwakalukwa, na kusema kuwa watoto hao ni wenye kati ya miaka 10 hadi 14.

“Hawa watoto walivunja nyumba ya Askari mstaafu na kuiba, Laptop 1, simu 1 na Solar pannel, walipohojiwa walikiri kuhusika na matukio ya wizi, tunaendelea kuwahoji ili tupate mtandao wao wote na kumaliza kabisa hili tatizo ambalo kwa sasa hapa Tabora limeanza kuibuka tena”, amesema ACP Mwakalukwa.

https://www.instagram.com/tv/CHSEKTahG7z/

https://www.instagram.com/tv/CHSEKTahG7z/

The post Watoto 11 wakamatwa kwa kuiba nyumbani kwa Askari (+ Video) appeared first on Bongo5.com.