Wasanii wa muziki wa dansi nchini wakiongozwa na Mama Asha Baraka wameweza kuungana na kukemea vikali vitendo vilivyotarajiwa kufanyika vya uvunjifu wa amani.

Wasanii hao wakioongozwa na Asha Baraka wameiomba Serikali kuhakikisha vitendo hivyo viovu visiweze kutokea kwani ni uvunjifu wa amani nchini.

Wameeleza kuwa Tanzania haikujengwa kwa ajili ya maandamano bali imejengwa kwa ajili ya amani na siku zote uchaguzi ni kama pambano la ngumi mmoja wao anaposhindwa haina budi kukubali na siku zote kwenye mbio mshindi lazima apatikane washindi hawawezi kuwa waili, bali kwa chama ambacho kimeshindwa kinatakiwa kujipanga kwa ajili ya uchaguzi ujao na sio kutangaza kuvunja amani, Sisi Watanzania amani ikipotea hatuna pa kukimbilia Tanzania ndio baba yetu Tanzania ndio amma yetu”

The post Wasanii wa dansi wakemea maandamano: Tanzania ndio baba ndio mama kwetu, hatuna pa kukimbilia (+Video) appeared first on Bongo5.com.