Maelfu ya wafuasi wa Rais Donald Trump wameandamana mjini Washington na kuimba nyimbo za kudai utawala wa "miaka minne zaidi" na kulaumu udanganyifu katika uchaguzi mkuu kama sababu ya kushindwa kwa Rais huyo.

Watu wasiopungua 10,000, ambao wachache walikuwa wamevaa barakoa, walikutana katika ukumbi wa Freedom Plaza kabla ya kuandamana hadi katika mahakama kuu huku wakipeperusha bendera za kumuunga mkono Trump.

Trump mwenyewe alionekana kuwaonyesha tabasamu wafuasi hao alipokuwa kwenye msafara wake akiwa njiani kuelekea kucheza gofu.

Kiongozi huyo wa chama cha Republican, bado anasisitiza madai ya kuwepo udanganyifu na kuwa alimshinda Rais mteule Joe Biden katika uchaguzi wa Novemba 3.