Wanafunzi 490,103 wanatarajiwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne, leo Novemba 23 ikiwa ni ongezeko la 0.9% la waliofanya mtihani hiyo 2019. Kati ya hao wavulana ni 213,553 (47%) wasichana ni 234,103 (52.3%)
Watahiniwa binafsi ni 41,939 wavulana wakiwa 18,118 sawa na 43.2% na wasichana 23,821 sawa na 56.8%

Wanafunzi wenye Uhitaji Maalum ni 893 ambapo 425 kati yao ni wenye Uoni Hafifu, 60 Wasioona, 186 Viziwi na 222 Walemavu wa Viungo

Jumla ya wanafunzi 9,426 wanatarajiwa kufanya Mtihani wa Maarifa (QT) ambapo wavulana ni 4,147 sawa na 44% na wasichana ni 5,279 sawa na 56%