Baadhi ya wanachama wa Chadema wakiwemo wajumbe wa Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha) wakiwa nje ya ofisi za makao makuu mtaa wa Ufipa, Dar es Salaam na mabango wakishinikiza chama hicho kuwafukuza uanachama makada 19 wa chama hicho ambao wameapishwa kuwa wabunge wa Viti Maalum mjini Dodoma bila idhini ya Chadema.

Wanachama hao 19 wakiongozwa na Halima Mdee ambaye ni mwenyekiti wa Bawacha leo Ijumaa Novemba 27, 2020 wanahojiwa na kamati kuu ya chama hicho kuhusu uamuzi wao wa kwenda kula kiapo wakati mchakato wa kupeleka majina yao ukiwa haujafanyika.