Walimu wawili wa  Shule ya Awali na Msingi ya Holly Cross Nursery iliyopo Temeke jijijini Dar es Salaam wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kudaiwa kumuua mwanafunzi wa Shule hiyo, Cathbert Chawe.

Washtakiwa hao ni, Leahdorice Agunda(35) na Maths Laizer ambaye ni Mkazi wa Mtoni Kijichi.
Wakisomewa hati ya mashtaka na wa Wakili wa Serikali Mwandamizi,Wankyo Simon  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Yusto Ruboroga amedai kuwa washtakiwa wanakabiliwa na shtaka moja ambao mnamo Septemba 14, 2020 katika shule ya awali na Msingi ya Holly Cross Nursery iliyopo maeneo ya Kijichi Wilaya ya Temeke wote Kwa pamoja wanadaiwa kumuua mwanafunzi wa shule hiyo, Cathbert Chawe huku wakijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria.
Wankyo amedai kuwa upelelezi wa shauri Hilo bado haujakamilika na hivyo aliiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Baada ya maelezo hayo Hakimu Ruboroga amesema washtakiwa hao hawarihusiwi kujibu chochote kwa kuwa kesi hiyo ni ya mauaji hivyo ameahirisha shauri hilo Hadi Novemba 19, mwaka huu.