Donald Trump amedai kuwa tayari ameshinda katika hotuba aliyoitoa katika ikulu ya White House hata kabla ya mamilioni ya kura kuhesabiwa.

Wachambuzi wa Republicans na wenye msimamo mkali hata hivyo wameonesha wasiwasi wao kuhusiana na matamshi yake.

Akizungumza na shirika la habari la ABC News, aliyekuwa gavana wa New Jersey na mshauri wa Trump Chris Christie ameitaja hatua ya Trump kama isiyofaa – hata kimkakati na kwake yeye kama rais.

“Ni uamuzi mbaya,” alisema. “Ni uamuzi mbaya wa kisiasa.”Rick Santorum, aliyekuwa Seneta wa Republican kutoka Pennsylvania, alisema kwamba matamshi ya Trump yamemsababishia “msongo wa mawazo”. “Kwa kutumia neno udanganyifu… kwangu naona ni makosa,” amesema hivyo akizungumza na CNN.

https://www.instagram.com/tv/CHKkkekBbxl/

https://www.instagram.com/tv/CHKkkekBbxl/

The post Wafuasi wa Trump wafadhaishwa na hotuba ya Trump, kudai kuna udanganyifu ni uamzi mbaya amenisababishia msongo wa mawazo (+Video) appeared first on Bongo5.com.