Mkuu wa ujumbe wa waangalizi wa kimataifa kwenye uchaguzi wa Marekani amesema jana kwamba madai ya Rais Donald Trump hayana msingi, yanayosema kwamba kumefanyika udanganyifu katika uchaguzi huo.
Michael Georg Link anayeongoza ujumbe wa Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya, OSCE ameongeza kuwa madai ya Trump yanadhoofisha imani ya umma kwa taasisi za kidemokrasia nchini humo.
Katika ripoti ya awali, ujumbe huo pia ulionya kwamba matamshi ya Trump wakati wa kampeni zake, yaliangaliwa na wengi kuwa na uwezo wa kuchochea vurugu za kisiasa baada ya uchaguzi.
Ujumbe huo pia ulitaka kuhesabiwa tena kwa kura zote baada ya timu ya kampeni ya Trump kusema kwamba imefungua mashtaka mahakamani ya kusitisha mchakato huo katika majimbo muhimu ya Michigan na Pennsylvania.
The post Waangalizi wa Kimataifa washindwa kumvumilia Trump appeared first on Bongo5.com.