Viongozi kutoka nchi tofauti za Afrika wamekuwa wakimpongeza rais mteule wa Marekani na makamu rais mteule, Kamala Harris, kufuatia ushindi wao wa uchaguzi mkuu.

“Natoa wito kwa Bw. Biden kutumia tajiriba yake kubwa kukabiliana na athari mbaya ya siasa ya utaifa katika masuala ya ulimwengu,” kiongozi wa Nigeria alisema.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni alitumai mkataba wa kibiashara utakaozipatia nchi za Afrika fursa ya kufikia soko la Marekani bila kutozwa kodi utatiwa saini upya.

Bi Harris alitajwa na rais wa Kenya kama “trailblazer” . Ameandikisha historia kama mwanamke wa kwanza, mwafrika wa kwanza na Mmarekani mweusi kuwa makamu wa rais wa Marekani.

Baadhi ya viongozi wa bara Afrika wamezungumzia rekodi ya bwana Biden na kukariri jinsi wanavyotazamia kufanya kazi na yeye.

Biden mweye umri wa miaka 77- alichaguliwa mara ya kwanza katika bunge la seneti la Marekani mwaka 1972 na kuhudumu kama makamu wa rais wa Barack Obama kwa miaka minane.

Nigeria: ‘Heshimu uamuzi wa watu’

Muhammadu Buhari, rais wa nchi ya Afrika iliyo na watu wengi zaidi na uchumi mkubwa, amesema ushindi wa bwana Biden umekuja “wakati ulimwengu

unakabiliwa na misokosuko mingi “.

Ruka Twitter ujumbe, 1

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

Kuchaguliwa kwake ni ishara kwamba demokrasia ndio mfumo mzuri zaidi wa serikali kwasababu unawapatia watu nafasi ya kubadilisha serikali kwa njia ya

amani,” Mr Buhari said.

Rais Trump bado hajakubali kushindwa na hajawahi kuzungumza hadharani tangu aliposhindwa.

“Kuheshimu uamuzi wa watu ndio sababu iliyofanya demokrasia kusalia kuwa mfumo mzuri wa utawala licha ya mapungufu kutoka kwa kigezo kimoja hadi

kingine, na kutoka jamii moja hadi nyingine,” Kiongozi wa Nigeria alisema.

Pia aliongeza kuwa Nigeria inatazamia kuwa na ushirikiano na Marekani” duniani – na badala yake kutoa wito kwa bwana Biden “kuanzisha ushirikiano mzuri na Afrika kwa kuzingatia maslahi ya Afrika na mahitaji yake”.

Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo pia alitoa wito wake na kuzungumzia fahari ya Afrika kumuona Bi Harris, aliyezaliwa na mama mhindi na baba Mjamaica

Kamala video

Sisi hapa barani Afrika tunajivunia sana ufanisi wake. Mwanamke wa kwanza mwafrika kuwa makamu wa rais. Rais wa kwanza wa Marekani mwafrika mwenye asili ya Kimarekani Barack Obama, alikuwa na chembe chembe ya vinasaba vya DNA ya Mkenya na ninaamini makamu wa rais mwanamke wa kwanza Mmarekani mwenye asili ya Kiafrika huenda akawa na DNA ya Mnaigeria kwasababu ya watu walioenda Caribbean kutoka Afrika ambayo ni Nigeria ya leo,” rais huyo wa zamani alisema.

Kenya: ‘Rafiki wa nchi yetu’

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alisema “ushindi” wa bwana Biden ulikuwa “ishara ya Wamarekani kuamini uongozi wa makamu wa rais wa zamani”.Joe Biden alizuru Kenya wakati alipokuwa makamu wa rais , hapa anakutana na wale walioathiriwa na bomu hilo la 1998 katika ubalozi wa Marekani

Rais mteule Joe Biden ni rafiki wa nchi yetu ambaye ashawahi kututembelea na kusaidia kuimarisha ushirikiano madhubuti kati ya Kenya na Marekani ,” katika taarifa rais Kenyatta alisema

“Ushindi wake unatoa fursa ya kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya nchi hizi mbili kwa ustawi wa watu wa nchi zetu mbili.”

Alisema Bi Harris atakuwa kielelezo chema na atasaidia kuwapa motisha mamilioni ya wasichana wadogo kote duniani kufikia ndoto yao ya kupata ufanisi maishani”.

Bwana Kenyatta pia alimshukuru bwana Trump kwa utawala wake na kusema “tunamtakia kila la heri anapojiandaa kuondoka madarakani kama rais wa Marekani”.

Uganda: ‘ombi la biashara’

Kiongozi wa Uganda Yoweri Museveni, alimtumia risala za heri njema bwana Biden na salamu kutoka kwa Waganda, kumkumbusha ushirikiano wa karibu wa nchi yake na Marekani.Ufadhili kadhaa umesimama afrika kutokana na hatua ya rais Trump kutofadhiliwa mashirika

“Marekani na jamii yake ya watu weusi milioni 47.4, pamoja na idadi kubwa ya waumini wa Kikristo inatuunganisha kwa njia ya imani, hali ambayo kwa uhalisia ni maisha ya Waganda na Waafrika kwa jumla ,” Rais Museveni aliweka ujumbe kwa tweeter.

“Marais wa zamani wa Marekani walitumia ushirikiano uliopo kwa kuweka sheria ya ukuaji na kuboresha nafasi ya biashara [Agoa]… Tunapongeza sera hiyo na kutumai kuwa Biden ataudumisha.”

Agoa ni sheria ya kwanza ya biashara ya Marekani iliyobuniwa kuimarisha biashara na uwekezaji kati ya Marekani na Afrika na uwekezaji kwa kutoa nafasi kwa nchi za Afrika kufikia masoko 6,500 ya uuzaji bidhaa nje ya nchi – muswada huo uliidhinishwa na Rais Bill Clinton mwaka 2000 na kuimarishwa zaidi na warithi wake George W Bush na bwana Obama.

Mkataba huo unamalizika 2025 na ikiwa hautawekwa saini upya huenda ukawa na athari kwa nchi ndogo na masikini.

Namibia: ‘ilipinga ubaguzi wa rangi’

Rais wa Namibia alisema nchi ambayo ilinyakua uhuru wake mwaka 1990 kutoka kwa utawala wa wazungu – wachache waliongoza Afrika Kusini baada ya vita vya miaka 25, alimshukuru bwana Biden kwa msaada wake wakati huo.

“Wakati wa harakati zetu za kupigania uhuru, tulimfahamu kama seneta aliyepinga ubaguzi wa rangi Afrika Kusini na eneo lote hilo,” President Hage Geingob alituma ujumbe wa twitter.

“Natazamia kufanya kazi na @JoeBiden kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kibiashara ili kutoa mazingira huru duniani.”

Liberia: ‘Sote tunakabiliwa na mzozo wa afya duniani’

George Weah, rais wa Liberia, moja ya nchi tatu zilizoathiriwa zaidi na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola Afrika magharibi mwaka 2014-16, akiangazia janga la corona alipokuwa akimtumia risala za heri njema Bw. Biden.

“Anachukuwa uongozi wa Marekani wakati nchi hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ya kiafya, hali ambayo pia inashuhudiwa kote duniani. Natoa wito kwa Wamarekani wote kusonga mbele pamoja kwa amani,” aliandika ujumbe kwenye tritter yake

“Kama washirika wa muda mrefu wa Marekani, Liberia iko tayari kufufua na kuimarisha uhusiano wetu wa biashara ya kihistoria . Pongezi!”

Misri: ‘Hatua ya pamoja’

Rais Abdul Fattah al-Sisi, mshirika wa karibu wa Bw. Trump ambaye ameunga mkono Misri katika mzozo wa ujenzi wa bwawa la mto Nile unaofanywa na

Ethiopia, alisema anatazamia kuwa na uhusiano kati ya nchi hizo mbili utaendelezwa na Bw. Biden.

“Rais alisisitiza umuhimu wa kuchukua hatua ya pamoja ili kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya Misri na Marekani, kwa maslahi ya nchi mbili rafiki na watu wake,” Shirika la habari la Reuters lilimnukuu msemaji wake akisema.

Zimbabwe: ‘Kuongeza ushirikiano’

Rais wa Zimbabwe, ambaye nchi yake imekuwa katika uhusiano wenye mvutano na Marekani kuhusiana na rekodi yake ya haki za binadamu, hakuchelea kumpongeza rais mteule.

Baadhi ya watu na wafanyabiashara wa Zimbabwe wamewekewa vikwazo ambavyo vimekuwa vimedumishwa kwa miaka 20 iliyopita .

“Zimbabwe inakutakia kila la heri katika uongozi wa watu Marekani. Natazamia kufanya kazi na wewe kuongeza ushirikiano kati ya nchi zetu mbili,” Rais Emmerson

Mnangagwa aliandika ujumbe wa Twitter.

Ghana: ‘umoja kwa Wamarekani wote’

Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo alielezea ushindi wa Bw. Biden “uamuzi mzuri” na kumpongeza Bi Harris kwa kuandikisha historia.

“Ni matumaini yangu kwamba hatamu ya Rais Mteule Biden uongozini italeta umoja, amani maendeleo na ustawi kwa Wamarekani wote,” aliandika kwenye

twtter yake.

“Nina matumaini kwamba uongizi wake, utaimarisha uhusiano ambao umekuwepo kwa miaka mingi kati ya Ghana na Marekani.”

Ethiopia, Niger, Senegal, Somalia na Afrika Kusini:

Viongozi wengine walituma ujumbe wao wa ponngezi siku ya Jumamosi baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, Rais wa Niger President Issoufou Mahamadou, Rais wa Senegal Macky Sall, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa

na Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed, maarufu Farmajo, walikuwa

miongoni mwa wale walioandika ujumbe katika mtandao wa Twitter wakisema wanatazamia kufanya kazi na Bw. Biden:

The post Viongozi Afrika wampongeza Rais mteule Marekani, Joe Biden  appeared first on Bongo5.com.