Mgombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Democratic nchini Marekani, Joe Biden kama atafanikiwa kuongoza  Nevada na Arizona atafikisha jumla ya kura 270 na kumuwezesha kuwa Rais wa taifa hilo kwa mujibu wa mtangazaji wa CNN, John King.

“Nevada na Arizona hayajaitwa lakini mpaka sasa Joe Biden anaongoza na Wolf  Blitzer kwa upande wake anaamini kama Joe Biden ataweza kuzilinda kura hizo za Nevada na Arizona atafanikiwa kupata kufikisha kura 270 hatakama hatofanikiwa kushinda Pennsylvania.”King.

Joe Biden amepiga hatua muhimu kuelekea kupata ushindi baada ya kunyakua majimbo tete ya Michigan na Wisconsin usiku wa kuamkia leo.

Katika taarifa fupi aliyoitoa akiwa pamoja na mgombea mwenza Harris Kamala, Biden amesema hawezi kujitangazia ushindi lakini ana matumaini kuwa zoezi la kuhesabu kura litakapomalizika wataibuka kuwa washindi. Kwa kunyakua majimbo hayo mawili, Biden amefikisha kura 264 za Baraza maalumu la wajumbe wanaomchagua rais dhidi ya 214 za rais Doanld Trump anayewania muhula wa pili.

The post Ushindi wa Joe Biden upo mikononi mwa Nevada na Arizona appeared first on Bongo5.com.