Mwimbaji Harmonize amewasha moto kwenye ukurasa wake wa Instagram, kilio chake kikubwa leo amekielekeza kwenye muziki wa bongo fleva.


Harmonize amesema muziki wetu umekosa utambulisho (sound), na kwa mtazamo wake anawapongeza Ma DJ wa bongo kwa kucheza ngoma za nje kwenye Club, hasa za wasanii wa Nigeria kwani inabidi watayarishaji na wasanii wa bongo fleva wabadilike na kuimba muziki wenye utambulisho wetu, akiupa kipaumbele muziki wa Singeli.


"Ninapenda namna Ma DJ wa Kitanzania hawachezi nyimbo zetu kwa wingi kwenye makumbi ya starehe, tunataja sana viungo vya pilau kwenye ngoma zetu. Hii ni nzuri, na ninajivunia. Inabidi tubadilike, tunawapa shida, waache kupiga (In My Maserati), (No Stress), (Woman), (Mapiano Sound), wakapige PEMBEMBELANG'OMBE, ukiuliza Uzalendo. Hatu promote, tunaiua Lugha yetu nzuri ya Kiswahili kwa aina mbaya ya muziki tunaoimba." aliandika Harmonize SWIPE kuona zaidi.