Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ujumbe huu:- Waziri Mstaafu!Alhamdulillah.
Kwanza, Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuhitimisha salama uwaziri wa Afya, Maendeo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kipindi cha 2015 – 2020.


.
Pili, kwa unyenyekevu mkubwa, ninamshukuru sana Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuniamini kuwa msaidizi wake wa kusimamia sekta ya Afya na Maendeleo ya Jamii ktk kipindi hiki. Asante sana Rais Magufuli. Hakika Nimejifunza mengi kutoka kwako. Umenifanya kusimama imara wakati wote kulinda maslahi ya Tanzania na watanzania.

Naamini wengi mtakubaliana nami kuwa sekta ya Afya ni moja ya sekta ambazo zimepata mafanikio makubwa ktk kipindi hiki cha Utawala wa Awamu ya 5, hii yote ni kutokana na utashi na dhamira ya dhati ya Rais Magufuli ya kutaka kuboresha maisha ya watanzania hususan wa kipato cha chini.

Tatu, Ninawashukuru watumishi wa sekta ya Afya na Maendeleo ya jamii wa ngazi zote nchi nzima kwa ushirikiano mzuri walionipatia ktk kutekeleza majukumu yangu. Nawashukuru kwa imani na upendo wao mkubwa kwangu. Siku zote wamekuwa wakiniamini na kuniheshimu licha ya kuwa sio mwanataaluma wa Afya. Asanteni sana. Ninawapenda. Mungu awabariki.

Nne,Katika utekelezaji wa majukumu yangu pia nimepata ushirikiano mzuri kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwemo sekta binafsi, mashirika ya kiraia na Wadau wa maendeleo wa ndani na nje ya nchi. Ninawashukuru sana kwa kuchangia mafanikio makubwa tuliyopata ktk sekta hii.

Tano, kwa watanzania wenzangu, asanteni sana kwa sala/maombi yenu na kwa ushirikiano mzuri mlionipa. Nimeona upendo wenu wa dhati kwangu hasa katika nyakati ngumu. Aidha ninawashukuru kwa kuzingatia maelekezo mbalimbali ya wataalam wa afya ya kulinda afya zenu. Ninawasihi sana tena sana tuendelee kuwekeza kwenye afya zetu. Ili kulinda na kuimarisha Afya zetu Tuzingatie ulaji wa vyakula unaofaa, kupunguza unywaji wa pombe kupita kiasi, kufanya mazoezi mara kwa mara #AfyaNiMtaji

Mwisho lakini sio kwa umuhimu ninakishukuru @ccmtanzania na wanawake wa UWT Mkoa wa Tanga kwa kunipa heshima ya kuwa Mbunge wa Viti Maalum kwa kipindi cha 2015-2020. Aidha, ninaishukuru familia yangu kwa kuniombea na kuwa nami bega kwa bega ktk kutekeleza majukumu yangu. Ninawapenda sana🙏

The post Ummy Mwalimu awashukuru Watanzania na wafanyakazi wa wizara ya afya appeared first on Bongo5.com.