Matokeo ya awali ya urais nchini Marekani kati ya Donald Trump na hasimu wake wa Democrat Joe Biden yanaonesha mchuano kuwa mkali katika majimbo kadhaa.

Donald Trump anaongoza katika jimbo la Florida kwa karibu kura zote zilizohesabiwa.

Lakini majimbo mengine ya Georgia, Pennsylvania, Wisconsin, Michigan, Arizona, Ohio, Texas, na North Carolina chochote kinatarajiwa.

Zaidi ya watu milioni 100 walikwisha piga kura zao za mapema.

Udhibiti wa Congress pia uko hatarini. Pamoja na Ikulu ya White House, Republican wanawania kupata idadi kubwa ya viti vya Seneti.

Bunge la wawakilishi linatarajiwa kuwa katika mikono ya Democratic.