Rais wa Marekani, Donald Trump, ameendelea kuibua mjadala zaidi baada ya kuandika kupitia ukurasa wake wa Twitter kwamba kuna mpango umeandaliwa wa kumuibia kura na wala hataruhusu jambo hilo lifanikiwe.


Matamshi yake yameamsha hisia zaidi nchini humo, huku akiongeza hofu ya kutokea kwa vurugu ikiwa atashindwa katika Uchaguzi huu. Awali alishatangaza kuwa huenda asikubaliane na matokeo ya Uchaguzi ambao anadai kuna njama za kumuibia kura.

Twitter imetoa tahadhari kuwa sehemu au chapisho zima la Trump linaweza kuwa la kupotosha kuhusu zoezi la Uchaguzi linaloendelea nchini humo.

The post Trump baada ya kuyaona matokeo ya mwanzo, adai kuna mpango wa yeye kuibiwa kura appeared first on Bongo5.com.