Rais Donald Trump wa Marekani amesema amemfuta kazi Mkuu wa Usalama wa Mtandao na Shirika la Usalama wa Miundombinu ya Uchaguzi (Cisa), Chris Krebs kwa taarifa zake “zisizo sahihi kwa kiwango cha juu kuhusu maadili ya kura”.

Trump amekataa kukubali kushindwa katika uchaguzi wa Marekani, akitoa madai yasiyo na ushahidi ya wizi mkubwa  wa kura.

Hata hivyo, Maafisa wa Uchaguzi wanasema kura ya mwaka huu ilikuwa moja ya kura salama zaidi  katika historia ya Marekani.

Wiki iliyopita Rais Trump alimfuta kazi Waziri wa Ulinzi, Mark Esper, huku kukiwa na ripoti kwamba alikuwa na wasiwasi juu ya utiifu wa mkuu huyo wa Pentagon.

Kumekuwa na tetesi mjini Washington DC kwamba kabla ya Trump kuondoka madarakani mwezi Januari, Mkuu wa CIA, Gina Haspel na mkurugeni wa FBI Christopher Wray huenda wakawa miongoni mwa wale watakaofutwa kazi na Trump.