KATIKA kumlinda kiungo wao mabosi wa Yanga, Kampuni ya GSM kupitia Mkurugenzi wa Uwekezaji, Injinia Hersi Said, wamefunguka kwamba watamuongezea mkataba kiungo wao Mukoko Tonombe raia wa DR Congo kutokana na kuwa na kipengele kinachowaruhusu kufanya hivyo.


 


Hersi ameongeza kwamba kipengele hicho cha kuongeza mkataba wa kiungo huyo, kiliwekwa wakati wanasaini mkataba wa kiungo huyo na mabosi wake, AS Vita.


 


Kiungo huyo ambaye ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Oktoba, amekuwa akihusishwa kutakiwa na Simba kwa ajili ya dirisha dogo. Hersi amesema kwamba nyota huyo na winga Tuisila Kisinda licha ya mikataba waliyonayo ya miaka miwili lakini muda wowote wanaweza kuongezewa pale mabosi hao watakapoona inafaa.


 


“Mukoko ana mkataba wa miaka miwili lakini kuna kipengele cha kumuongezea mkataba sisi Yanga ambacho tulikisaini kwenye mkataba kule AS Vita.


 


“Yeye (Mukoko) na Kisinda (Tuisila) mikataba yao ina hicho kipengele, lakini mkataba wake hauna ruhusa ya klabu yoyote ile kuuvunja,” alimaliza Hersi.