Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limetoa ufafanuzi kuhusiana yanayoendelea kuwa Rais wa TFF Wallace Karia ni mfaidika wa pesa za Rais wa CAF Ahmad Ahmad ambazo zimemfanya afungiwa na FIFA kwa miaka mitano na faini ya Tsh milioni 510.1.

TFF imesisitiza kuwa ni kweli ziliwahi kutumwa dola 100,000 (Tsh milioni 231.8) ambazo ziliidhinishwa na kamati ya utendaji ya CAF May 2017 na kutaka dola 80,000 (Tsh milioni 185.5) zitumike TFF kwa ajili ya kuendeleza soka na dola 20,000 (Tsh milioni 46.3) zilizobaki ziende kwa Wallace Karia kwa kusaidia shughuli zake za kiutendaji kwa kuwa hana mshahara.