Kiungo wa kati Mjerumani Sami Khedira, 33, anasema anaweza kuhamia katika Primia Ligi wakati mkataba wake na Juventus utakapoisha msimu huu.

Aliongeza kuwa anaendelea kuwasiliana na mameneja wa Everton Carlo Ancelotti na wa Tottenham Jose Mourinho. (ZDF, via Mail)

Mkataba wa mlindalango wa AC Milan Gianluigi Donnarumma katika Serie A unamalizika mwaka 2021 lakini kijana huyo wa kimataifa Muitaliano mwenye umri wa miaka 21- anasema wakala wake ataongea na klabu na anataka kuendelea kubakia nao kwa "muda mrefu". (Football Italia)

Liverpool wamekuwa wakihusishwa na mlinzi wa Ajax Perr Schuurs, 21, lakini the Reds hawajafanya dau lolote kwa ajili ya Mholanzi huyo . (Voetbal Primeur - in Dutch)

Celtic wanataka kumsaini kiungo wa kati wa Crystal Palace na Jamuhuri ya Ireland James McCarthy, lakini Aston Villa na Burnley pia wanamtaka kijana huyo mwenye umri wa miaka 30. (Teamtalk)

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anasema "hashiri sana kuhusu wale watakaoingina na kutoka " wakati wa dirisha la uhamisho la wachezaji la mwezi wa Januari . (Evening Standard)

Viungo wa safu ya kati Wahispania Riqui Puig, 21, na Carles Alena, 22, wanapijgania hali zao za baadaye katika timu ya Barcelona sawa na mshambuliaji Mdenmark Martin Braithwaite, 29, na kiungo wa nyuma-kushoto Muhispania Junior Firpo, 24. (Marca)

Winga wa Ufaransa Florian Thauvin anasema ali "ondolewa " na mkurugenzi wa masuala ya kiufundi wa AC Milan Paolo Maldini akisema timu hiyo ya Serie A side iliitaka kumsaini . Mkataba wa kijana huyo mwenye umri wa miaka 27-katika timu ya Ufaransa ya Marseille unaisha msimu ujao wa soka wa mwaka 2021. (Football Italia)

Juventus wanaweza kumlenga kiungo wa safu ya kati-nyuma wa Atletico Madrid na kiungo wa kati -nyuma wa Montenegro Stefan Savic, 29,ili kuimarisha safu yao ya ulinzi. (Calciomercato)

Kiungo wa zamani wa safu ya nyuma-kushoto wa Brazil Roberto Carlos amesema mpango wake wa kuhamia Chelsea ulio "afikiwa" mwaka 2007 na ulivunjwa tu katika "nyakati za mwisho ". (Goal)

Barnsley wanaangalia kwa makini uwezekano wa kurefisha mkataba wa mkopo wa Leicester City kumuhusu mchezaji wa safu ya kati Matty James katika klabu hiyo, huku mkataba wa Muingerezaq huyo mwenye umri wa miaka 29 ukitarajiwa kumalizika mwezi wa Januari . (Leicestershire Live)