Manchester City wameazimia kusaini mkataba na mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi, 33, baada ya meneja Pep Guardiola kukubali mkataba mpya. (Mirror)

Manchester United watapambana na Paris St-Germain na Real Madrid katika kumsaini kiungo wa kati Mfaransa mwenye umri wa miaka 18 kutoka klabu ya Rennes Eduardo Camavinga. (Marca, via Mail)

Klabu kadhaa za Ligi ya Primia zinataka kumsaini beki wa uhispania Sergio Ramos, iwapo kijana huyo mwenye umri wa miaka 34 hataongeza mkataba wake Real Madrid . (90min)

Real Madrid watamnunua beki wa Bayern Munich na Austria David Alaba, 28, kama Ramos ataondoka au la (Marca)

Everton wanaangalia uwezekano wa kumsaini winga Manchester United na Wales Daniel James, 23, mwezi January. (Football Insider)

Mshambuliaji Olivier Giroud, 34, yuko tayari kuangalia uwezekano wa ofa ya kuondoka Chelsea mwezi Januari kwa lengo la kuendelea mchezo wake katika kikosi cha Ufaransa kwa ajili ya msimu ujao wa kombe la Ulaya. (Guardian)

Newcastle United wako tayari kusikia ofa kwa ajili ya kiungo wa kati wa Paraguay Miguel Almiron, 26, ambaye tayari amepewa ofa za klabu kadhaa. (90min)