Nyota wa muziki nchini, Aslay Isihaka ameingia kwenye headline baada ya kuchukua tuzo (plaque) NNE kwa pamoja kutoka kampuni ya ku-stream muziki ya Boomplay.

Aslay amekabidhiwa Tuzo hizo Alhamisi hii, kufuatia kwa EP yake, "Kipenda Roho" kufikisha streams zaidi ya milioni 1, ndani ya mtandao huo, huku nyimbo zake "Likizo" pamoja na "Natamba" kufikisha streams zaidi ya Laki 5.


Aslay pia kapata Plaque (tuzo) ya Streams zote alizofikisha kwenye app ya Boomplay, ambayo ni plaque ya stream zaidi ya milioni 5. Kwa hatua hiyo kubwa, #Aslay anaungana na wasanii kama #Mbosso, #Jux pamoja na #Nandy ambao nao ndani ya mwaka huu wameweza kupata Tuzo (plaque) kutoka Boomplay.