Spika wa Bunge Jamhuri wa Muungano aliyemaliza muda wake Job Yustino Ndugai, amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi kumpendekeza kuwa Spika wa Bunge la 12.

Spika wa Bunge Jamhuri wa Muungano aliyemaliza muda wake Job Yustino Ndugai

Ndugai amechukua fomu yakuomba ridhaa leo katika ofisi za chama mara baada ya taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole, ya kuwaalika wanachama wenye sifa stahiki kwa mujibu wa sheria kuanza kuchukua fomu za kuomba ridhaa.

Naye Mbunge mteule wa jimbo la Mbeya Mjini Tulia Ackson, ambaye alikuwa Naibu Spika wa Bunge la 11 amechukua fomu ya kukiomba chama cha CCM, kumpendekeza kuwa Naibu Spika katika Bunge la 12.

Aidha baaada ya zoezi la uchukuaji na urejeshewaji wa fomu hizo kamati za Siasa za Halmashauri Kuu za CCM za Wilaya zitakaa kikao na kutoa mapendekezo yao dhidi ya mchakatao huo.

Ikumbukwe kuwa fomu zinazochukuliwa ni Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Naibu Spika, Meya wa Halmashauri ya Jiji na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya.

The post Spika Ndugai na Naibu wake Tulia Ackson wachukua fomu kutetea viti vyao appeared first on Bongo5.com.