SIMIYU: Majangili wakamatwa meno mawili ya Tembo na fuvu lake (+Video)

Jeshi la polisi mkoani Simiyu, linawashikilia watu wawili wakazi wa Kijiji cha Longalombogo wilayani Itilima mkoani humo, baada ya kuwakuta na meno mawili ya Tembo pamoja na fuvu lake, wakiyasafirisha kupeleka Kahama mkoani Shinyanga kwenda kuyauza.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu, ACP Richard Abwao

Hayo yamebainishwa hii leo Novemba 4, 2020, na Kamanda wa Polisi mkoani humo, ACP Richard Abwao, na mara baada ya kuwatia nguvuni watuhumiwa hao walikiri na kudai kuwa wameyaokota katika pori la akiba la Maswa.

“Askari wa kikosi maalum waliongozwa na watuhumiwa hadi eneo la tukio na kukuta mabaki ya mnyama huyo, wataalamu wa wanyamapori wanaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha kifo cha Tembo huyo, haya meno yalivyo inaonekana huyu Tembo alikuwa ni mkubwa kwa sababu kwenye jino moja walitoa vipande vinne”, amesema ACP Abwao.

The post SIMIYU: Majangili wakamatwa meno mawili ya Tembo na fuvu lake (+Video) appeared first on Bongo5.com.