Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), limetangaza matokeo ya kumaliza elimu ya msingi uliofanyika tarehe 7 na 8 Oktoba 2020.

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde leo Jumamosi tarehe 21 Novemba 2020, yanaonyesha kati ya shule kumi bora zenye watahiniwa zaidi ya 40, Dod’s Bridge ya jijini Mbeya inaongoza kundi hilo huku Mkoa wa Kagera ikiingiza shule mbili.

Dk. Msonde, amebainisha shule kumi ambazo kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo, zimeongeza ufaulu ambapo Mwandu Kisesa ya Mkoa wa Simiyu imeongoza kundi hilo.

Katibu mtendaji huyo, amezitaja shule kumi ambazo kwa miaka mitatu mfululizo, zimeshuka ufaulu kwa kiasi kikubwa ikiongozwa na Chororo naya mwisho ikiwa Ng’ongolo zote za Mtwara.