Cristiano Ronaldo anafikiria kurejea Manchester United baada ya klabu hiyo ya Premier League kuanza mazungumzo ya kutaka kumsajili tenya mchezaji huyo, kwa mujibu wa ripoti mbalimbali.

Mreno huyo mwenye umri wa miaka 35, kwa sasa ni msimu wake wa tatu tangu kujiunga na Juventus akitokea Real Madrid mwaka 2018.

Ripoti za hivi karibuni zimedai kuwa Paris Saint-Germain imeanza kuonesha nia ya kutaka kumsajili nyota huyo wa Juventus.

Lakini kwa mujibu wa ESPN Argentina na mwandishi wa habari wa Fox Sports Argentina, Christian Martin amedai kuwa United imeshaanza mazungumzo na Ronaldo.

Ronaldo ametumia miaka sita ndani ya United akitokea Sporting Lisbon akiwa na umri wa miaka 18 nmwaka 2003 chini ya Sir Alex Ferguson, Ronaldo amekuwa moja kati ya wachezaji wakubwa duniani na kuisaidia United kutwaa mataji matatu ya Premier League, FA Cup na Champions League.

Mwaka 2008, Ronaldo akawa mchezaji wa kwanza ndani ya United kushinda taji la Ballon d’Or tangu kufanya hivyo  George Best mwaka 1968.

United ilimuuza Ronaldo kwenda Real Madrid mwaka 2009 kwa dau la paundi milioni 80, huko alikwenda kujenga ufalme wake vema huku akipatiwa changamoto na Lionel Messi.

Mzee Ferguson aliwahi kujaribu kutaka kumrudisha Ronaldo kutokea Madrid kabla hajaachana na soka mwaka 2013 lakini United ilishindwa kukamilisha dili hilo.

IMEANDIKWA NA HAMZA FUMO, INSTAGRAM @fumo255

The post Ronaldo huyoo Manchester United appeared first on Bongo5.com.